kaisa079
Joined
Sep-17-2011
Gender

Hometown

Age

Interest(s)
About Me
Nilizaliwa katika kijiji cha Nyang’ombe kata ya Nyamagaro wilayani Rorya. Nilipata elimu ya msingi katika shule mbali mbali zikiwemo Nyamagaro (Rorya), Rwamlimi (Musoma Mjini), Shimbale (Bariadi) na elimu ya sekondari katika shule ya Ihungo (Bukoba) na Sengerema mkoani Mwanza na elimu ya kidato cha tano na sita katika shule ya Tabora wavulana mkoani Tabora. Nilipata shahada ya Udaktari katika Chuo cha sayansi za tiba cha Muhimbili na kufanya kazi katika Hospitali ya Mwananyamala kwa muda kabla ya kufanya kazi katika Shirika la World Vision na Shirika la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation kwa vipindi tofauti. Nilianza kuandika kitabu hiki nikiwa katika chuo cha sayansi za tiba cha Muhimbili na kurasa za nusu ya mwisho zimeandikwa wakati nikiwa katika chuo kikuu cha sayansi yya afya ya jamii cha Johns Hopkins Bloomberg , Baltimore, Maryland nchini Marekani nimesoma shahada ya juu ya sayansi ya afya ya jamii. Yote yaliyoandikwa humu yamefanyiwa utafiti wa kina kwa miaka zaidi ya mitano.
Social Network Settings
Favorite Choices

Visit Personal Bookstore: Personal Bookstore